Tuesday, 14 February 2017
Arusha: Watu 80 watiwa mbaroni kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya
Jeshi la polisi mkoani Arusha linawashikilia watuhumiwa 80 akiwemo askari moja wa polisi kwa kujihusisha na biashara ya dawa za kulevya
Aizungumza na wanahabari ofisini kwake, Kamanda wa Polisi Mkoa wa Arusha, Charles Mkumbo amesema kuwa msako uliofanyika mwanzoni mwa mwezi huu umefanikisha kukamata misokoto 3,845 ya bangi na mirungi Kilogramu 33 pamoja na kete 167.
Alisema, “Katika misako hiyo ambayo ilifanyika wilaya zote sita za mkoa huu, watuhumiwa 54 walipatikana kwenye tuhuma za bangi, 14 ni tuhuma za Heroin na 12 ni wa tuhuma za mirungi.”
Alifafanua, “watuhumiwa 40 ni wauzaji wa madawa hayo huku 13 ni wale ambao walikuwa wanajihusisha kwa namna moja au nyingine na bangi na mmoja alikuwa anasafirisha. Watuhumiwa 14 wa Heroin kosa lao kupatikana huku 12 makosa yao ni kupatikana na mirungi na hivyo kufanya idadi yao kuwa 80 ambao ni wanaume na wanawake.”
Aidha Kamanda wa Polisi aliwashukuru wananchi wa mkoa huu kwa ushirikiano wa utoaji wa taarifa za uhalifu na kuwaomba waendelee kufanya hivyo.
Subscribe to:
Post Comments (Atom)
No comments:
Post a Comment