Wednesday 1 March 2017

Idris Sultan: Mimi ni mmoja wa celebs wa Bongo wanaoongoza kwa ‘big deals’ (Video)



Mambo yanazidi kumnyookea Idris Sultan.


Muigizaji, mchekeshaji na mtangazaji huyo amesema kuwa yeye ni mmoja wa mastaa wa Tanzania wenye mikataba mingi minono ya matangazo. Anadai kuwa deals nyingi anazipata kutokana na namna anavyoitumia mitandao ya kijamii kutengeneza utani unaowachekesha wengi.
“Hiyo imenipa deals nyingi. Nadhani kuanzia mwezi wa nane mwaka jana mpaka mwaka huu, I think ninaweza nikawa moja kati ya celebrities wa Bongo ambao wanaongoza kwa big deals,”
“Ingawaje sijataja figures zozote in which sipendi lakini nimeweza kufanya deals kubwa mpaka sasa hivi nafanya na Tecno, nafanya na Halotel, nafanya na MeTL, hapa nyuma kuna kazi za MTV pia nilipata, nilipata gig ya kuhost show kubwa Uganda. I think vimekuja haraka haraka sana because how flexible nipo,” ameongeza.
Idris anasema kazi za filamu pia zimekuwa zikimuijia ikiwemo Kiumeni inayotoka mwezi huu na amedai kuwa kuna filamu nyingine ya Rwanda


No comments:

Post a Comment