Wednesday 1 March 2017

Kocha wa Barcelona Enrique aweka wazi mpango wake wa kujiuzulu kuifundisha timu hiyo




Kocha wa klabu ya Barcelona Luis Enrique ametangaza kwamba atabwaga manyanga mwishoni mwa msimu huu.

Enrique atakuwa amehudumu kama meneja wa klabu hiyo kwa misimu mitatu.
Aliishindia klabu hiyo kombe la vilabu bingwa na mataji mengine mawili alipojiunga na Barcelona na kuwasaidia kushinda makombe 2 mwaka uliopita.
Lakini licha ya klabu hiyo kuongoa katika jedwali la ligi Barcelona iko katika hatari ya kubanduliwa katika kombe la vilabu bingwa Ulaya msimu huu baada ya kufungwa 4-0 na Prais St-Germain.
Enrique amesema kuwa sababu kuu ya yeye kutaka kujiuzulu ni kwamba anahitaji kupumzika.


No comments:

Post a Comment