Sunday, 9 April 2017

Aliyepeleka Mabomu Uganda Yaliyoua Watu 76 ajulikana Alikuwa Mtanzania!...!!!?



Mkurugenzi Mkuu wa Taasisi ya Kuzuia na Kupambana na Rushwa (TAKUKURU), Valentino Mlowola amesema wakati anateuliwa na Rais John Magufuli alikuwa nchini Uganda kutoa ushahidi katika kesi ya ugaidi inayomkabili mtu aliyemkamata hapa nchini kwa tuhuma za mauaji ya watu 76 nchini humo.

Amesema kwamba, mtuhumiwa aliyekuwa akitoa ushahidi dhidi yake anadaiwa kuua watu 76 nchini Uganda waliokuwa wakiangalia michezo ya Kombe la Dunia kupitia televisheni.

“Hata wakati napewa taarifa ya kuja kuongoza chombo hiki nilikuwa mahakamani natoa ushahidi wa kesi ambayo Waganda 76 waliuawa katika shambulio wakati wa World Cup (mashindano ya kombe la dunia), kwa sababu mtuhumiwa aliyepeleka mabomu Uganda alikuwa Mtanzania.

“Na nilimkamata kwa mikono yangu Arusha, nikatakiwa nikatoe ushahidi kule wakati natoa ushahidi ndio nikapigiwa simu na Katibu Mkuu Kiongozi wakati ule Ombeni Sefue akinijulisha tukutane ili anipe taarifa ya kuongoza chombo hiki.” alisema.


No comments:

Post a Comment