Tuesday 11 April 2017

Ronaldo kama Messi tu, naye hatiani kuikosa El Classico.

Image result for MESSI NA RONALDO

Hadi sasa ni wazi Neymar atakosa mchezo ujao kati ya Barcelona na Real Madrid (El Classico), Neymar alipewa kadi nyekundu wakati wa mchezo kati yao na Malaga.
Wakati Neymar akiukosa mchezo huo, kwa upande wa Real Madrid Pepe naye yuko hati hati kuikosa El Classico baada ya kuumia mbavu wakati wa mchezo wao dhidi ya Atletico Madrid.
Sasa Cristiano Ronaldo naye yuko katika hati hati za kuukosa mchezo huo, Ronaldo anadaiwa kumfokea muamuzi wa mchezo wao dhidi ya Atletico baada ya kuona anawaonea.
Inasemekana wakati Ronaldo akimkaripia muamuzi huyo, alitoa maneno ambayo sii mazuri mbele ya muamuzi huyo jambo ambalo ni utovu mkubwa wa nidhamu katika soka.
Gazeti la michezo nchini Hispania liitwalo Sport limedai kitendo alichofanya Ronaldo hakina tofauti kubwa na alichofanya Messi na kupendekeza adhabu kali itolewe kwa Ronaldo sawa na ile aliyopewa Lioneil Messi.
Huu huenda ukawa mwaka wa majanga kwa Ronaldo kwani hata fomu yake uwanjanj imeporomoka sana, na sasa anawafanya mashabiki wa Real Madrid kuwa na hofu kwani mara zote Ronaldo amekuwa muhimu katika El Classico.


No comments:

Post a Comment