Tuesday 11 April 2017

Kombe la Dunia kuziweka meza moja Marekani na Mexico

Sio kwa kila jambo watu wanaweza kuwa maadui kuna wakati mwingine yapo mambo ambayo yanawaunganisha mahasimu ambapo leo April 11, 2017 nimekutana na hii ya Kombe la Dunia kuziunganisha Marekani na Mexico.
Unaambiwa nchi za Marekani, Mexico na Canada zimeungana pamoja kwa ajili ya kuomba kuandaa Fainali za Kombe la Dunia 2026 katika tangazo walilolitoa April 10 kwenye mkutano ulioandaliwa na Mashirikisho ya Soka ya nchi hizo tatu mjini New York.
Itakumbukwa kuwa Mexico na Marekani ziliingia kwenye mgogoro baada ya Rais wa sasa wa Marekani, Donald Trump, kutaka kujenga ukuta baina ya nchi hizo.
“Tuna support kubwa kutoka Serikali ya Marekani kwenye mpango huu. Rais wa Marekani anatusapoti na kututia moyo katika jambo hili. Amefurahi kwamba Mexico ni sehemu ya mpango huu.” – Rais wa Shirikisho la Soka Marekani Sunil Gulati.
Shirikisho la Soka Duniani, Fifa, linatarajia kumtangaza muandaaji wa Fainali za Kombe la Dunia 2026 ifikapo May 2020 ambao utakuwa mwaka wa mwisho wa kipindi cha kwanza cha Trump. Na hata hivyo kwa mujibu wa ukomo wa urais wa Marekani, Trump hatokuwa pia ofisini mwaka 2026.
“Rasmi! USA, Canada na Mexico zimeazimia kupeleka maombi ya kuandaa 2026 FIFA World Cup.” -U.S Soccer.




No comments:

Post a Comment