Tuesday 11 April 2017

Sadio Mane kuwa nje kwa miezi miwili



Mchezaji wa klabu ya Liverpool Sadio Mane, anafanyiwa operesheni ya goti siku ya leo Jumanne, na atakosamechi zote zilizo salia za msimu huu wote.
Aliumiza gegedu la goti lake la kushoto, baada ya kugongana na Leighton Baines kwenye mechi yao walioichezea katika uwanja wao wa nyumbani iyoishia 3-1 dhidi ya Everton.
Kocha Jurgen Klopp amesema kuwa Mane, mwenye umri wa miaka 25, anahitaji upasuaji, na kufanya kuwa “vigumu kwake kucheza msimu huu”.
Liverpool iko katika nafasi ya tatu kwenye msimamo wa ligi ya Uingereza, huku ikisalia na mechi sita tu.
Jeraha hilo litamfanya kukaa nje ya uwanja kwa miezi miwili ijayo.
Mane ambaye alijiunga na klabu hiyo kwa kitita cha Paundi milioni 34 kutoka timu ya Southampton msimu uliopita, na amecheza mechi zote sita za Liverpool msimu huu.
Katika mechi hizo, walishinda mchuano mmoja, tatu wakatoka sare na wakapoteza mechi mbili


No comments:

Post a Comment