Saturday 3 June 2017

UCHAMBUZI NA HISTORIA ZA TIMU ZOTE HIZI MBILI NA SHAFFIH DAUDA KUELEKEA FINALI ZA UEFA CHAMPIOS LEAGUE MTOTO HATUMWI DUKANI

Image result for uefa real vs juventus
Dunia itasimama kwa muda ili kushuhudia fainali ya aina yake ya UEFA Champions League kati ya Real Madrid vs Juventus usiku wa leo Juni 3, 2017 kwenye mji wa Cardiff.
Shaffih Dauda ametoa uchambuzi wake kuelekea mchezo huo ambao utafatiliwa na mamilioni ya wapenda soka Duniani kote.
Huu ni uchambuzi wake binafsi na maoni yake kuelekea mchezo huo haimaanishi kila kitu kitakuwa kama anavyoamini yeye ila pia inaweza ikatokea kama anavyotarajia.
Juventus ndio timu pekee iliyoruhusu mabao chache kwenye michuano ya Champions League, imefungwa mabao matatu tu katika mechi 12 walizocheza hadi sasa.
Walifanilkiwa kuizuia Barcelona isifunge goli hata moja katika dakika 180 (mechi mbili) nyumbani na ugenini katika hatua ya robo fainali. Hiki ni kitu kizuri kwao na utaona ni jinsi gani walivyo na safu bora ya ulinzi wakiongozwa na golikipa wao mkongwe Gigi Buffon pale langoni, Bonucci, Barzagli na Chiellini wanatengeneza ukuta mgumu kupitika.
Real Madrid wameshafunga magoli 32 hadi sasa kwenye mechi zao za Champions League msimu huu, wakati Juventus wao wamefunga magoli 21 huku timu zote zikiwa zimecheza mechi 12.
Christiano Ronaldo kwa misimu sita mfululizo, anafunga mabao 10 na zaidi kwa hiyo amekuwa mfungaji mahiri katika michuano hii. Ronaldo amekuwa akimuonea Gianluigi ‘Gigi’ Buffon mara zote ambazo wawili hao wamekutana, Ronaldo ameweza kumfunga.
Katika fainali 5 zilizopita za UEFA Champions League ambazo Real Madrid walifanikiwa kucheza, wameshinda fainali tano, mara ya mwisho Real Madrid kupoteza mchezo wa fainali ya mabingwa wa Ulaya ilikuwa ni mwaka 1981 walikalishwa na Liverpool.
Fainali walizoshinda Madrid ni pamoja na 1998 walishinda dhidi ya Juventus, 2000 wakaifunga Valencia, 2002 wakaichukua kwa kuifunga Liverkusen, 2014 wakaifunga Atletico Madrid na kuchukua kombe na 2016 wakalitwaa tena.
Wakati Madrid wakishinda fainali 5 zilizopta ambazo walifanikiwa kucheza, kwa upande wa Juve kwao mambo ni tofauti kabisa. Wapeigwa katika fainali 4 zilizopita ambazo wamefanikiwa kufika hivi karibuni.
Fainali ya 1997 Juve walichezea kichapo kwa Dortmund, 1998 wakakaa kwa Real Madrid, 2003 wakapigwa tena na AC Milan, 2015 wakapoteza kwa Barcelona.
Fainali ni fainali na rekodi zipo ili kuleta msisimko, lakini nikiwaangalia Juve kwa jinsi walivyojengeka kwenye nafasi ya ulinzi kweli wapo vizuri lakini inategemea wanacheza na nani.
Real Madrid wana options nyingi, Gareth Bale asipokuwa sawa anaweza akacheza Isco na timu ikacheza kulingana na uwepo wa Isco na usione pengo la Bale.anaweza asicheze Benzema akacheza Morata, Danilo na Carvajal pia unaweza usione tofauti.
Juve wao wanajivunia kuwa na kuwa na kikosi cha kwanza bora, mechi yao ya fainali dhidi ya Real Madrid sitoshangaa kumuona Juan Cuadrado akianza ili kumnyima nafasi Marcelo ya kupanda juu kushambulia. Juve wakiwachezesha Dani Alves na Cuadrado katika upande wa kulia wanakuwa na nguvu sana na upande huo ndio Madrid wana nguvu kwa sababu ya Marcelo na Ronaldo.


No comments:

Post a Comment